Nia yetu tupendane wawili,
sikatai lakini kuna jambo linalo huzunisha,
naogopa wanaokupenda watanipa taabu mimi'
hali ya unyonge sijiwezi...
ukweli nakupenda lakini naogopa.
usiogope wala usitie shaka,
tafadhali usiniwache pweke,
wewe ndio mpigo wa roho yangu,nitaishije bila wewe???
hao wengine hawana maana yoyote maishani mwangu,
wewe pekee ndio kipenzi cha roho yangu.....
elewa mpenzi kama tutapendana,
wapo wengi wabaya watakao jaribu kututenganisha,
usiyaache maneno yao yaje kati yangu mimi na wewe,
wewe ni ua la roho yangu....kipenzi cha maisha yangu
naomba usiniweke pembeni lazizi,
ingawa wapo wengi wazuri...
nilikuchagua wewe!!
tabia zako sawa na sura yako,
nimeridhika kuwa na wewe mami....
wewe ni sabuni wa moyo.....mpigo wa roho yangu!!!
nitawezaje kuishi bila wewe???
No comments:
Post a Comment